Looking for something in our website? Search here

Utaratibu wa M4P

AMDT inatumia Mchakato wa M4P kwenye kazi zake. Kwa kufata utaratibu huu, mkazo unawekwa zaidi kwenye ukuaji na matokeo ya kudumu kwenye jamii na kuongeza thamani kwenye maisha ya watu. Jiunge nasi katika jitihada hizi.

1: Tathmini ya Masoko

Changanua kwa Utafiti

AMDT hutathamini mifumo ya masoko, ikiwemo miradi ya sasa na ya zamani ndani yake ili kuweza kuchanganua na kufahamu changamoto za kimkakati na vyanzo vyake. katika hatua zote, AMDT inazingatia tathmini ya usawa wa jinsia na jinsi changamoto huathiri wanaume, wanawake na vijana. Hii huwezesha kuelewa aina ya utatuzi kwa kila changamoto na kundi lake. Pia masuala ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa huzingatiwa katika tathmini hizi.

Tafiti za tathmini huwezesha uchanganuzi wa changamoto ambazo AMDT yaweza kuwekeza katika kuwezesha utatuzi wake. AMDT inatambua kwamba haiwezi kushughulikia changamoto zote kwenye mifumo ya masoko, lakini inazingatia kuweka vipaumbele kwenye maeneo ambayo yataleta matokeo makubwa yenye faida kwa walengwa na wadau wengi. Mwisho, ili kuzuia marudio na kuboresha msingi wa taarifa na maarifa , AMDT itazingatia uorodheshwaji wa miradi yote, ya zamani na ya sasa katika kila sekta ndogo ya kilimo.

2: Jaribu Ubunifu

Jaribu Suluhisho na Tathmini Matokeo

AMDT inafanya kazi kwa ubia na wadau wa sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi yake, huku ikizingatia utatuzi wa changamoto zilizochanganuliwa, mazingira na pia masuala mazima ya mabadiliko ya tabianchi na usawa wa kijinsi.
Wadau wanahimizwa kuweka ubunifu katika miradi ya majaribio katika kushughulikia changamoto za mifumo ya masoko ya sekta za kilimo.

Miradi itakayopewa kipaumbele itategemea vigezo maalum vya tathmini ikiwemo kugusa jamii maskini, kuleta thamani tarajiwa na fursa za kusambazwa eneo kubwa zaidi. Pia inazingatiwa matokeo chanya na uwezo wa kugusa maisha ya wanawake na vijana, utunzaji mazingira na kuzingatia mabadiliko ya tabianchi. AMDT itatathmini na kuthibitisha kwanza matoke ya miradi ya majaribio. Matokeo hafifu kwenye hatua ya majaribio haitachukuliwa kama kushindwa, badala yake linakua somo kwa upangaji na utekelezaji wa miradi hiyo baadae. Maarifa na maandiko haya yatatangazwa na kusambazwa kwa wadau wengi wa sekta pana ya kilimo nchini Tanzania kupitia shughuli za uratibu wa maarifa na mawasiliano hapa AMDT.

3: Jaribu Miradi

Sambaza Matokeo na Tathmini

Miradi ya majaribio itafuatiliwa kwa karibu ili kuona maeneo yanayoweza kurekebishwa kuleta matokeo chanya. Majaribio yatakayoonyesha mafanikio tarajiwa na kuonyesha mweleko wa matokeo chanya hata kwa kiwango kidogo yatakua na nafasi kupata uwekezaji ili kutanua zaidi miradi hiyo na kufaidisha watu wengi.

Kutakua na muendelezo kwenye tathmini na ufuatiliaji matokeo kwa miradi ya majaribio na ile mikubwa ya uwekezaji. Taarifa na maarifa yatakayokusanywa zitatumika kuratibu mwelekeo wa miradi na pia kusaidia maamuzi ya AMDT kwa miradi ya siku zijazo. Pia maarifa na maudhui yatakayopatikana yatatumika katika kazi za Uratibu wa Maarifa na Mawasiliano hapa AMDT ikiwemo mafunzo, kusambaza kupitia vyombo mbalimbali nk.

4: Kituo cha Maarifa

Uendeshaji na Uratibu

AMDT inawekeza kwenye kuwa kituo muhimu cha kutumia, kufundisha na kuhamasisha Mfumo/Utaratibu wa M4P kwenye katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini Tanzania. Kupitia miradi yake, AMDT inategeneza, kukusanya na kutafiti maudhui, habari, data na maarifa mengi kwa ajili ya mafunzo na mwongozo vinavyosaidia wadau wengi katika sekta ya kilimo.

Kupitia jitihada hizi, AMDT itaanzisha na kuweka umadhubuti kwenye Kituo cha Maarifa ambacho lengo lake hasa litakua ni kusambaza maarifa, maudhui na data kwa wadau na umma kwa njia rafiki na zenye tija zaidi. Pia, AMDT itajitolea na kujiweka katika nafasi ya kuhimiza na kusukuma jitihada za pamoja katika kuendeleza sekta ya kilimo kwa kushirikiana na wadau wote ikiwemo wa kimkakati wakiwemo serikali katika kuboresha mazingira ya biashara za kilimo