Looking for something in our website? Search here
Kuinua wakulima wadogo

Kusukuma mapinduzi ya Sektamama ya Kilimo kukuza uchumi

Uboreshaji wa maeneo muhimu ya mifumo ya masoko ya sekta za Kilimo kupitia uwezeshaji unaodumu

Stack
International team

AMDT Kwa Ufupi

Uchumi wa Tanzania unaendeshwa kwa Kilimo huku 80% ya jamii maskini zikiishi maeneo ya vijijini. Pamoja na umuhimu wake kwenye Uchumi wetu, bado mchango wa uzalishaji kwenye Kilimo kwa kila Mtanzania ni mdogo sana na kati ya viwango vidogo zaidi duniani. Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania -II (Mkukuta II) unatambua umuhimu wa Kilimo na unahimiza sana mapinduzi kwenye SektaMama hii. Pia, Sera ya Taifa ya Kilimo Kwanza inatoa mwongozo, sera za usimamizi na maeneo ya kimkakati ya kuwekeza Kitaifa. Lengo kuu likiwa kuongeza tija na uzalishaji, na kuhimiza uongezaji thamani hapa hapa Tanzania ili kutoa fursa za ajira kwa wananchi. Matokeo yake ni kupambana na umaskini kwa vitendo.

Serikali ya Tanzania na Wadau wa Maendeleo wanakubali kuwa ukuaji wa Sekta ya Kilimo utasukumwa zaidi na Sekta Binafsi kupitia kwa viwanda vidogo na vya kati (MSMEs) ambavyo ndio vitakua kiungo muhimu cha sekta. Viwanda hivi ndio hutoa huduma za pembejeo, ukuzaji biashara, na kusukuma biashara ya kuuza-kununua mazao, uongezaji thamani, ufungashaji na biashara ya bidhaa za kilimo. Fursa za biashara kwenye kilimo bado kabisa hazijaguswa kikamilifu nchini Tanzania. Juhudi za mwanzoni kuinua sekta hii hazikua na muunganiko na hivyo kutofikia malengo kwa ukubwa unaotegemewa ili kugusa maisha ya jamii kubwa ya watu maskini, wote wanawake na wanaume.

Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT) ni ya KiTanzanian, ikiwa imeanzishwa ili kwezesha uratibu mzuri wa miradi katika sekta za kilimo, kuboresha uelewa na tija kwenye mifumo ya masoko, kuinua tija na upatikanaji masoko kwa viwanda vidogo na vya kati, yote hii ili kuongeza matoke chanya na kutoa mchango madhubuti kwenye mapambano dhidi ya umaskini nchini Tanzania.

+0

Available developers

+0K

Clients Every Year

+0M

Revenue in 2020

+0

Staff members in Europe

+0K

Food Produced

+0K

Acres Harvested

+0M

Support Given

+0

Awards Won

Wanufaika wa Miradi

Walengwa wa uwezeshaji wa AMDT kwenye kilimo ni jamii maskini za nguvukazi za wanawake, wanaume na vijana wengi wao wakiwa wakulima wadogo na wanaojishughulisha na uzalishaji kwenye sekta za kilimo. Hawa ni pamoja na vibarua na watu wanaojiajiri.

Nguvukazi ya watu maskini kwa AMDT ni jamii inayoanzia wale wanaotumia Dola za Marekan 0.74 kwa siku (ambao hujulikana kama watu walio kwenye kiwango kikubwa cha umaskini) mpaka wale wenye ahueni kiasi juu ya mstari wa umaskini (wa matumizi ya Dola za Marekani 1.25 kwa siku) au kiwango cha umaskini cha Taifa). AMDT haiweki kipaumbele kwa kwa jamii za maskini wa kutupwa wasio na nguvu ya uzalishaji, ingawa mfumo wa uwezeshaji wa AMDT unaleta mabadiliko yanayokwenda kugusa maisha ya jamii hizi kupitia fursa za ajira na kipato.

Njia Tuliyochagua: Maono na Dhima

Miradi yetu inajenga ukuaji katika jamii kwa uwezeshaji unaodumu

Our Mission is to unleash large scale systemic change in agricultural market systems such that productive poor women, men and youth are able to take advantage of more inclusive, resilient and competitive market systems. AMDT believes that enabling large scale systemic change targeting market systems critical for the productive poor, creates a much stronger chance of achieving sustained pro-poor impact.

AMDT envisions an agricultural sector where productive poor women, men, and youth in Tanzania have increased and sustained income and employment opportunities.

Development Partners